Home Soka Akaminko Asimamishwa Azam Fc

Akaminko Asimamishwa Azam Fc

by Sports Leo
0 comments

Taarifa za ndani kutoka katika klabu ya Azam Fc zimethibitishwa kwamba kiungo wa klabu hiyo James Akaminko amesimamishwa kushiriki shughuli zote za klabu hiyo kutokana na utovu wa nidhamu na ndio sababu kuu ya  kutoonekana kikosini Kiungo huyo raia wa Ghana.

Imefahamika kuwa James Akaminko amekuwa na maelewano hafifu na kocha wake mkuu Dabo kwa kipindi kirefu kabla ya siku kadhaa zilizopita kusimamishwa kukitumikia kikosi hicho mpaka pale uongozi utakapotoa taarifa rasmi kwa staa huyo baada ya uchunguzi kukamilika na hatua stahiki kuchukuliwa.

Kiungo huyo amekua mhimili mkubwa kwa Azam Fc tangu asajiliwe klabuni hapo msimu wa 2022/2023 ambapo baada tu ya kucheza mechi kadhaa na klabu hiyo alizivutia klabu za Simba sc na Yanga sc ambapo msimu uliopita Yanga sc iliwasilisha ofa ya kutaka kumsajili rasmi kiungo huyo.

banner

Kocha Dabo amekua muumini mzuri wa nidhamu kwa mastaa wa timu hiyo ambapo mara kadhaa ameingia matatizoni na baadhi ya mastaa kama Sospeter Bajana kutokana na utovu wa nidhamu kikosini humo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited