Home Soka Aussems Awa Mbogo

Aussems Awa Mbogo

by Dennis Msotwa
0 comments

Kocha wa Simba sc Patrick Aussems alikua mkali na mwenye hasira baada ya kutoka katika kikao na viongozi wa klabu hiyo kilichofanyika katikati ya jiji la Dar es salaam zilizopo ofisi za mtendaji mkuu wa klabu hiyo Senzo Mazingisa.

Kocha huyo alionekana akifoka huku akiwa ameambatana na msaidizi wa tajiri wa klabu hiyo Barbra Hernandez huku akiwa mwenye hasira kali.

Kocha huyo aliitwa kujieleza baada ya kusimamishwa kwa siku kadhaa kufuatia kuonesha utovu wa nidhamu baada ya kuondoka nchini bila kutoa taarifa rasmi huku tetesi zikidai alikwenda kufanya mazungumzo na baadhi ya klabu ikiwemo Polokwane Fc ya afrika ya kusini.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited