Kocha wa Simba sc Patrick Ausems ameonyesha ubabe baada ya kuisadia timu hiyo kuibuka na ushindi katika mechi nne za ligi kuu ilizocheza mpaka sasa ambapo kufuatia ushindi huo mfululizo amepata tuzo ya kocha bora wa mwezi Septemba.
Mbeligiji huyo alioongoza Simba sc katika mechi tatu za mwezi septemba ambapo Kati ya michezo hiyo mmoja nyumbani dhidi ya Mtibwa Sugar na miwili ugenini mabao 3-0 dhidi ya Kagera Sugar na mabao 2-0 dhidi ya Biashara United na kuifanyaSimba kumaliza mwezi ikiwa nafasi ya kwanza.
Kocha huyo amewafunika Mohammed Rishard wa Prisons na Abdallah Mohammed Baresi wa JKT Tanzania ambapo ameshinda michezo yote huku Baresi aliingoza JKT Tanzania kushinda michezo miwili, sare moja na kupoteza mmoja wakati Richard akifanikiwa kuiongoza Prisons kushinda michezo miwili na kutoa sare mmoja, ambapo ilishinda nyumbani mabao 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting, kisha ikashinda ugenini mabao 3-1 dhidi ya Mtibwa na ikatoka sare ugenini na Lipuli ya mabao 2-2.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.