Home Soka Azam Fc Wajichimbia Kileleni Nbc

Azam Fc Wajichimbia Kileleni Nbc

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Azam Fc imeendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi kuu nchini baada ya kufanikiwa kuifunga mabao 4-0 klabu ya Kagera Sugar Fc katika mchezo wa ligi kuu nchini uliofanyika katika uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.

Iliwachukua Azam Fc dakika 9 kufunga bao la kwanza kupitia kwa Feisal Salum kwa shuti kali akimalizia pasi ya Idd Nado ambapo dakika mbili baadae Prince Dube naye akaongeza bao la pili la mchezo huo akiunganisha vizuri pasi ya Paschal Msindo na dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza Pascal Msindo aliongeza bao la tatu.

Kipindi cha pili Kagera Sugar walitulia na kuanza kucheza kwa tahadhari kubwa lakini tayari jahazi lilishazama na Alasane Diarra alimalizia kalamu ya ushindi kwa bao dakika ya 84 ya mchezo huo.

banner

Azam Fc sasa imefisha alama 31 katika mechi 13 za ligi kuu nchini huku Yanga sc wakiwa katika nafasi ya pili wakiwa na alama 27 baada ya kucheza michezo 10 ya ligi kuu na Simba sc wenyewe wako nafasi ya tatu ya msimamo na alama 22 katika michezo 9 huku Kagera Sugar wakiwa nafasi ya 13 na alama 13.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited