Waoka mikate wa Chamazi Azam Fc imeanza ligi kuu Tanzania Bara kwa kulazimishwa sare ya 1-1 na Coastal Union katika mchezo uliofanyika katika dimba la Mkwakwani jijini Tanga.
Azam walijipatia goli lake dakika ya 48 kipindi cha pili kupitia kwa beki Daniel Amoah akiunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu uliopigwa na Idd Suleiman.Zikiwa zimesalia dakika chache kutamatika kwa mchezo huo beki Hance aliisawazishia Coastal na kubakiza alama moja katika uwanja wa nyumbani.
Sare hiyo imeendeleza rekodi ya Coastal Union kupoteza mchezo wa ligi dhidi ya Azam wakiwa Mkwakwani.
Katika mchezo wa kwanza uliochezwa mchana Mbeya Kwanza wameiduwaza Mtibwa Sugar kwa ushindi wa 1-0 katika dimba la Mabatini Ruvu huku Wauaji wa Kusini Namungo wakiichabanga Geita Gold kwa magoli 2-0 yaliyofungwa na Shiza Kichuya na Reliant Lusajo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Ligi hiyo itaendelea hapo kesho ambapo mabingwa watetezi Simba itakuwa Mara kukabiliana na Biashara United katika uwanja wa Karume.