Home Soka Azam Fc yaifunga 1-0 Ihefu Fc

Azam Fc yaifunga 1-0 Ihefu Fc

by Sports Leo
0 comments

Bao la Feisal Salum Dakika ya 13 ya mchezo kati ya Azam Fc dhidi ya Ihefu Fc limetosha kuipatia alama tatu klabu yake hiyo katika mchezo wa ligi kuu baina ya timu hizo uliofanyika katika uwanja wa Chamazi jijini Dar es salaam.

Azam Fc iliyokua ikitafuta alama hizo muhimu ili kuendelea kujichimbia katika nafasi ya pili hasa baada ya Simba sc kupoteza mbele ya Yanga sc siku ya Jumamosi hivyo kutumia fursa hiyo kuzoa alama ili kujiweka pazuri zaidi katika msimamo wa ligi kuu.

Feisal alifunga bao hilo akipokea pazi ya Nathaniel Chilambo baada ya kazi nzuri ya Gibril Sillah upande wa kulia mwa uwanja huo na kuwaacha mabeki ya Ihefu Fc wakilaumiana kutokana na kutokaba vizuri.

banner

Azam Fc sasa imefikisha alama 54 katika michezo 24 ya ligi kuu nchini ambapo Ihefu Fc sasa imesalia katika nafasi ya 11 ya msimamo ikiwa na alama 25 katika michezo 24 ya ligi kuu ya soka nchini.

Feisal Salum mpaka sasa ameendelea kutoa upinzani mkali katika orodha ya wafungaji akiwa na mabao 14 pamoja na assisti sita katika ligi kuu msimu huu.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited