Home Soka Azam fc yakubali kumwachia Sure Boy

Azam fc yakubali kumwachia Sure Boy

by Dennis Msotwa
0 comments

Uongozi wa klabu ya Azam fc hatimaye wamekubali ombi la kiungo wao Salum Abubakar  ‘’sure boy’’ kuondoka katika klabu hiyo yenye makazi yake Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam baada ya kuitumikia kwa muda mrefu tangu alipojiunga nayo mwaka 2007.

Hayo yamethibitishwa na Afisa habari wa Azam fc Zaka Zakazi akisema kuwa wamepokea bbarua rasmi ya mchezaji huyo kupitia kwa mtendaji mkuu Nurdin Popat ambaye aliipeleka kwa wanasheria wao walioipitia kwa kuangalia vipengele vya mkataba.

Baada ya hapo walipelekea ombi hilo kwa bodi ya klabu hiyo ambayo wamekubali bila kinyongo kusitisha rasmi mkataba wa mchezaji huyo mwandamizi ndani ya kikosi hicho,hatua hiyo ya kumuachia huru bila gharama yoyote ni kulipa fadhila kwa mchezaji huyo kwa kuitumikia klabu hiyo kwa mafanikio makubwa.

banner

Zaka Zakazi amesema kuwa Sure Boy ataendelea kuwa nembo ya timu hiyo na siku zote ataendelea kuwa kijana wao hivyo wameamua kuachana pasipo kuwa na shari,pia wamemtakia kila la kheri huko anakoenda.

Mchezaji huyo anaenda kujiunga na Yanga katika dirisha hili dogo la usajili,timu ambayo ilitumikiwa na baba yake mzazi mzee Abubakar Salum,na usajili wake ni kutimia kwa ndoto za wanachama na mashabiki wa Yanga ambao walitamani kijana huyo arejee nyumbani.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited