Home Soka Azam Fc Yanogewa kwa Straika

Azam Fc Yanogewa kwa Straika

by Dennis Msotwa
0 comments

Klabu ya Azam fc imeamua kumuongezea mkataba mpya mshambuliaji wake mpya raia wa Ivory coast Richard Djodi baada ya kukoshwa na kiwango chake alichokionesha hivi karibuni.

Staika huyo aliyesajiliwa kutoka Ashanti Gold ya Ghana ameicheza Azam fc mechi tatu na kufunga mabao mawili amewavutia mabosi hao waliomuongezea mkataba mpya ambapo sasa atadumu chamazi mpaka mwaka 2022.

banner

Katika taarifa iliyotolewa na Azam fc kupitia ukurasa wao wa mtandao wa facebook picha zinamuonesha mchezaji huyo akisaini mbele ya mtendaji mkuu wa timu hiyo Abdulkarim Amin “Poppat”.

“Tunayo furaha kutangaza kuwa tumefikia makubaliano ya kuingia mkataba mpya wa miaka miwili zaidi na kiungo mshambuliaji, Richard Djodi”.Ilisomeka taarifa hiyo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited