Home Soka Azam Fc Yanogewa na Mustafa

Azam Fc Yanogewa na Mustafa

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Azam FC ipo katika hatua za mwisho za kumsajili moja kwa moja mlinda lango wake Mohamed Mustapha ambaye yupo klabuni hapo kwa mkopo akitokea katika klabu ya Al Mereikh ya Sudan.

Mustapha alisaini mkataba wa mkopo wa miezi sita na Azam ila baada ya kufurahishwa na kiwango chake wanataka kumsajili moja kwa moja kuchukua nafasi ya makipa waliomajeraha Ali Ahmada na Idrissou Abdulai ambao wanatarajiwa kurejea mwishoni mwa msimu huu.

Kutokana na kiwango bora cha kipa huyo ambaye alikuja kuziba nafasi baada ya kipa Zubeiry Foba kushindwa kuziba pengo la makipa wa kigeni ambapo inatarajiwa Ali Ahmada anaweza kuachwa moja kwa moja ili kutoa nafasi kwa Mustapha klabuni hapo.

banner

Azam Fc inajenga kikosi cha kutwaa ubingwa wa ligi kuu nchini ambao hawajautwaa kwa takribani miaka kumi sasa na tayari wameanza maboresho ya kikosi kwa kusajili mastaa wawili eneo la kiungo na sasa ni zamu ya kuimarisha eneo la golikipa.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited