Taarifa za ndani ni kuwa uongozi wa Azam Fc umetuma ofa kwa kocha mkuu wa KMC Fc Abdulhamid Moalin arejee kwa mara nyingine ndani ya viunga vya Azam Complex kuchukua nafasi ya kocha Yousouph Dabo.
Inasemekana tayari ilishatuma ofa ya kwanza kwa Kocha Abdulhamid Moalin ambayo ameikataa baada ya kuwa na maslahi ambayo bila shaka Kocha Moalin ameona hakuna sababu ya kuiacha KMC FC ambayo inashika nafasi ya tatu kwenye ligi.
Baada ya kocha huyo kutojibu ofa hiyo klabu hiyo iliamua kuiboresha na kuituma tena huku KMC Fc mpaka sasa wakiwa hawajui la kufanya kutokana na sababu kwamba ofa ya Azam Fc kwa kocha huyo ni kubwa hivyo ni ngumu kumzuia.
Moalin amekua na mwendelezo mzuri kwa timu ya Kmc aliyojiunga nayo akitokea Azam Fc msimu huu ambapo ameiongoza kuifunga Mtibwa Sugar jana na kuifanya Kmc kupanda mpaka nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi kuu nchini.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Azam Fc ambao jioni ya leo watawavaa Mashujaa Fc wanahaha kutafuta kocha mpya baada ya timu hiyo kutokua na mwenendo usioridhisha ambapo mpaka sasa wamepoteza michezo miwili mfululizo dhidi ya Yanga sc na Namungo Fc wakiwa katika nafasi ya nne ya msimamo wa ligi kuu ya Nbc.