Home Soka Bacca Gumzo Afcon 2024

Bacca Gumzo Afcon 2024

by Sports Leo
0 comments

Beki wa klabu ya Yanga sc Ibrahim Bacca amekua gumzo katika michuano ya mataifa ya Afrika ambayo inaendelea nchini Ivory Coast ambapo sasa imeingia katika hatua ya 16 bora baada ya hatua ya makundi kumalizika na hatimaye kupatikana timu hizo ambazo zitawania kuingia robo fainali.

Licha ya Tanzania kutolewa katika michuano hiyo mawakala wengi wa soka pamoja na maskauti wa timu mbalimbali waliopo nchini humo wamekua mara kwa mara wanaulizia jina la beki huyo mali ya klabu ya Yanga sc ambao alisaini nao mkataba mpya wa miaka mitatu mpaka mwaka 2027.

Stars imeyaaga mashindano hayo ikiambulia alama mbili tu baada ya kufungwa na Morocco huku itikitoa sare dhidi ya Zambia na Drc Congo na kuifanya ishike nafasi ya mwisho katika msimamo wa kundi F.

banner

“Maskauti watatu mpaka sasa wamefika kambini kumuulizia Bacca lakini kati yao wawili ndio wapo siriazi mana wamekuja zaidi ya mara moja kuulizia kuhusu taarifa zake hvyo nategemea kusikia taarifa nzuri kutoka kwa klabu yake kuangalia kama ofa zitakua zimefika”.

Bacca katika kikosi cha Taifa Stars amefanikiwa kucheza mechi zote tatu akicheza kama mlinzi wa kati sambamba na Bakari Nondo Mwamnyeto huku akionyesha uwezo mzuri wa kukabiliana na washambuliaji hatari barani Afrika.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited