Bayern Munich bado wana nia ya kupata saini ya winga Leroy Sane kutoka Manchester City licha ya kuyumba kwa uchumi kutokana na janga la virusi vya corona .
Mkurugenzi wa Michezo wa Bayern Hasan Salihamidzic siku ya jumapili alisema kwamba klabu yake ina mpango wa kusajili vipaji viwili vya hali ya juu katika dirisha la usajili akiwemo Sane .
Bayern wanataka kulipa kuanzia kiasi cha Pauni Milioni 52 mpaka 60 , majira ya kiangazi yaliyopita alikuwa na thamani ya Pauni Milioni 87.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.