Home Soka Beki Yanga Kuwakosa Shooting

Beki Yanga Kuwakosa Shooting

by Sports Leo
0 comments

Beki wa Yanga sc Paul Godfrey “Boxer” ataukosa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting kufuatia majeruhi aliyoyapa kwenye mechi ya kimataifa ya klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Township Roller baada ya kutonesha misuli.

Beki huyo aliyepandishwa kutoka kikosi cha vijana cha timu hiyo na kubadilishwa nafasi kutoka winga mpaka beki na kocha Mwinyi Zahera aliumia katika mchezo wa kwanza  uliofanyika nchini August 10 na licha ya kupona alijitonesha katika mchezo wa pili mjini Gaborone licha ya kumalizia dakika 90 za mchezo.

Kwa mujibu wa daktari wa Yanga sc mchezaji mwingine atakayekosa mchezo huo ni beki Ally Ally aliye majeruhi na Juma Mahadhi mwenye majeraha ya goti.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited