Kocha Mkuu wa Simba SC, Abdelhak Benchikha amesema kuwa anapambana kwa moyo wake wote ili kuhakikisha timu hiyo inachukua ubingwa wa Ligi kuu Tanzania Bara pamoja na kufika mbali kwenye Ligi ya Mabingwa barani Afrika.
“Nimekuja Tanzania kushinda mataji na nimeridhishwa na usajili ambao tumefanya hivyo Simba ya kesho ni nzuri,”Alisema kocha huyo mwenye rekodi ya kutwaa taji la kombe la shirikisho barani Afrika baada ya kuifunga Yanga sc.
Benchika tangu atue Simba sc ameonyesha msisitizo hasa katika suala la nidhamu ambapo amewasimamisha wachezaji Cletous Chama na Nassoro Kapama ambaye tayari ameondoshwa kwa mkopo kikosini humo huku akisajili majembe ya kazi kurudisha furaha kwa mashabiki wa Simba sc.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Usajili wa Omar Pa Jobe,Fredy Michael,Edwin Balua,Babacar Sarr unatajwa kuwa ni moja ya mapendekezo ya kocha huyo ili kuja kuleta ushindani wa kutosha katika ligi kuu nchini.