Home Soka Benchika Atinga Tatu Bora

Benchika Atinga Tatu Bora

by Sports Leo
0 comments

Kocha wa mpya wa Simba Sc Abdelhak Benchikha ameingia katika orodha ya makocha watatu bora wanaowania tuzo za CAF 2023 ambazo zitafanyika Jumatatu Desemba 11 jijini Marakechi nchini Morocco.

Kocha huyo amefanikiwa kuingia katika hatua ya fainali akishindana na Walid Regraui ambaye ni kocha wa timu ya Taifa ya Morocco na Alidu Cisse ambaye ni kocha wa timu ya taifa ya Senegali kuwania tuzo hiyo.

Benchika ameingia katika tatu bora baada ya kuwa na msimu mzuri uliopita akiwa kocha wa klabu ya Usm Algers ambapo alifanikiwa kutwaa mataji ya kombe la Shirikisho akiifunga Yanga sc pamoja na kombe la super Cup alipomfunga 1-0 Al Ahly Fc.

banner

Msimu huu kocha huyo amejiunga na klabu ya Simba sc kwa mkataba wa miaka miwili ambapo kazi yake ya kwanza ni kurudisha kiwango cha timu hiyo ambayo imekua na matokeo ya kusuasua huku ikiwa na ndoto ya kufika nusu fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited