Home Soka Biashara Wafuzu Kimataifa

Biashara Wafuzu Kimataifa

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Yanga SC kwa sasa rasmi imeungana na klabu ya Simba kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya klabu Bingwa Afrika (CAF Champion League) msimu wa 2021/22 baada ya kuifunga Ihefu kwa magoli 2-0 na kufikisha pointi 73 na kuwa na uhakika wa kumaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ya Vodacom,

Vilabu vya Azam FC na Biashara United vyenyewe vitaiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya kombe la shirikisho (CAF Confederation Cup) baada ya kuwa na uhakika wa kumaliza nafasi ya 3 na 4 kwenye msimamo wa ligi kuu ya Vodacom

Biashara Utd leo walikuwa wakihitaji alama moja mbele ya Tz Prison ndiyo ambayo wameipata baada ya kutokka sare 1-1 katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliomalizika jioni ya leo huku timu ya Mwadui ikiwa tayari imeshuka daraja na Coastal Union na Ihefu fc pamoja na Mtibwa Sugar zikipambana kutoshuka daraja.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited