Aliyekua kocha mkuu wa klabu ya Alliance ya jijini Mwanza Athuman Bilal “Billo”ameamua kuachana na klabu hiyo baada ya kuiongoza katika mechi moja ya ligi kuu pekee.
Kocha huyo aliyejiunga na timu hiyo akitokea Stand united ya mjini Shinyanga ameachana na klabu hiyo kwa madai ya kukataa kuingiliwa majukumu yake.
“Nilitaka kuondoka kabla ya mechi na Mbao fc lakini nikatumia busara zangu Kubaki na kukiongoza kikosi cha Alliance kwa mechi hiyo tu moja, kwani nilitaka kulinda heshima yangu kwa kuachana na klabu hiyo ambayo ni ngumu mno kuifundisha.”alisema Billo
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Billo ni miongoni mwa makocha maarufu jijini Mwanza na kanda ya ziwa kwa ujumla kutokana na kufanikiwa kuzifanya timu anazozifundisha kuwa ngumu kufungika hasa zinapocheza na timu kubwa kama Simba na Yanga.