Shirikisho la soka barani Afrika (Caf) limegomea ombi la timu ya Township Rollers la kubadili uwanja utakaofanyika mchezo dhidi ya Yanga sc kutoka uwanja wa taifa wa Botswana kwenda uwanja mwingine mdogo.
Awali Township Rollers walipanga mchezo ufanyike katika uwanja wa taifa wa nchi hiyo wenye hadhi sawa na uwanja wa taifa wa hapa nchini lakini baada ya kuona hawana rekodi nzuri katika uwanja huo waliamua kubadilisha na kutaka kuhamishia mchezo huo kwenye uwanja mdogo walioubatiza jina la machinjioni.
Uamuzi huo wa CAF ni habari njema kwa Yanga kwani sasa watacheza kwenye uwanja sawa na huu wa Taifa ambao waliutumia kwenye mchezo wa kwanza.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Yanga wanatakiwa washinde ama wapate sare ya kuanzia magoli mawili ili kusonga mbele baada ya kutoka sare ya bao moja kwa moja nchini.