Shirikisho la Soka Afrika CAF limeruhusu Wachezaji wa Al Merrikh SC, Ramadan Agab na Bakhit Khamis kucheza mechi dhidi ya Simba baada ya awali kuwa na sintofahamu kuhusu uhalali wa wachezaji hao.
Kwa mujibu wa CAF wachezaji hao walifungiwa kucheza mashindano ya ndani lakini hawakatazwi kushiriki Mashindano ya CAF hivyo wako huru.
Awali shirikisho la soka nchini Sudan liliwafungia wachezaji hao kutokana na kusajiliwa na timu mbili za ndani hivyo suala hilo liliwafanya Simba sc kutuma malalamiko Caf kudai alama za mezani kutokana na wachezaji hao kuchezeshwa kinyume na taratibu.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.