Mshambuliaji wa Manchester United Edinson Cavani amefungiwa kutocheza michezo 3 pamoja na faini ya kiasi cha £100,000 kwa neno lake la kibaguzi alilolitoa katika mtandao wa Instagram dhidi ya shabiki yake.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Psg amefungiwa kwa kosa la kupost mtandaoni kwa kutumia neno linaloashiria ubaguzi. Neno hilo ni ”Negrito”Cavani atakosa mchezo dhidi ya Aston Villa (PL), Man City (EFL Cup) na Watford (FA Cup).