Home Soka Chama Aibeba Simba sc

Chama Aibeba Simba sc

by Sports Leo
0 comments

Kiungo Cletous Chama wa Simba scameibuka shujaa baada ya kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Mbeya Kwanza katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Mbeya kwanza walicheza mchezo huo kwa nidhamu kubwa huku wakikaba mtu na nafasi na hatimaye kufanikiwa kwenda mapumziko timu zikiwa bila bila.

Kipindi cha pili iliwalazimu Simba sc kusubiri mpaka dakika ya 85 ya mchezo kupata bao hilo lililolalamikiwa na wachezaji wa mbeya kwanza kuwa ni Offside baada ya Meddie Kagere kuingilia mchezo akiwa eneo la kuotea na kumfanya mwamuzi kumpa kadi ya njano Rolland Msonjo wa Mbeya kwanza kwa utovu wa nidhamu.

banner

Simba sc sasa imefikisha alama 31 ikiwa nafasi ya pili ya msimam0 huku Yanga sc wakiwa kileleni na alama 36 huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited