Home SokaChan 2025 Samia Achangia 200m Kuiua Morocco

Samia Achangia 200m Kuiua Morocco

by Dennis Msotwa
0 comments

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan amewapa wachezaji wa Taifa Stars kiasi cha Shilingi Milioni 200 ili wahamasike kuelekea kwenye mchezo wa robo fainali ya CHAN 2024 dhidi ya Morocco utakaofanyika siku ya ijumaa katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.

Taifa Stars inakabiriwa na kibarua kigumu katika mchezo huo wa robo fainali ya michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani dhidi ya Morocco ambao wana kikosi imara chenye wachezaji wengi vijana na wenye vipaji vya hali ya juu.

Samia Achangia 200m Kuiua Morocco-sportsleo.co.tz

banner

 

Stars ilianza michezo yake hiyo ikiwa katika kundi B lenye timu za Burkina Faso,Mauritania,Madagascar na Central Afrika ambapo katika mchezo wa kwanza iliibaimiza Burkina Faso kwa mabao 2-0 kisha ikiifunga Mauritania kwa mabao 2-1 na ikashinda 1-0 dhidi ya Madagascar lakini ilibanwa na kutoa sare katika mchezo wa mwisho wa makundi dhidi ya Central Afrika.

Kutokana na kanuni za Shirikisho la soka barani Afrika mshindi wa kundi B hukutana na washindi wa juu wa kundi A ambapo Tanzania kama kinara wa kundi B inakutana na Morocco iliyomaliza katika nafasi ya pili ya kundi A ambalo Kenya alikua kinara wa kundi hilo.

Hii si mara ya kwanza kwa Rais Samia kutoa fedha kwa ajili ya Taifa Stars ambapo katika michezo yote ya Chan kila goli alikua akilinunua kwa shilingi milioni kumi ambapo zimekua zikitolewa papo kwa papo.

Mpaka sasa kampeni mbalimbali zinaendelea ili kuhamasisha mashabiki kujitokeza kwa wingi kwenda uwanjani kuangalia mchezo huo ambao bei za tiketi zimeshushwa mpaka kufikia shilingi elfu mbili za kitanzania ambapo pia baadhi ya Taasisi na makampuni yameanza kununua na kugawa tiketi bure ili mashabiki wajaze uwanja.

Kwa mujibu wa taratibu za usalama za Shirikisho la soka barani Afrika (Caf) mashabiki elfu arobaini na moja na mia tisa pekee ndio wanaruhusiwa kuingia uwanjani kw kununua tiketi huku maeneo mengine yakiachwa kwa sababu za kiusalama zaidi.

Taifa Stars mbali na kupokea zawadi hiyo kutoka kwa Rais kama motisha pia Azam Tv imeahidi kutoa shilingi milioni hamsini kama zawadi endapo itafuzu kwenda nusu fainali na benki ya Nmb nayo itachangia kiasi cha shilingi milioni kumi kama zawadi ikiwa ni nje na dau la Wizara inayohusika na michezo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited