Klabu ya Chelsea chini ya mkufunzi Frank Lampard imeendelea kung’ang’ani nafasi nne za juu katika msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza baada ya kufanikiwa kuifunga Crystal Palace mabao 3-2.
Mabo ya Chelsea yalipatikana kupitia kwa Oliver Giroud dakika ya 6,Christian Pulisic dakika ya 47 na Tabby Abraham dakika ya 71 huku yale ya Palace yakifungwa na Wilfred Zaha dakika ya 34 na Christian Benteke dakika ya 72.
Chelsea wamepanda mpaka nafasi ya tatu wakiwa na alama 60 huku Leicester City wakiwa nafasi ya nne kwa alama 59 na nafasi ya tano inashikiriwa na Man united wenye alama 55 wakiwa na mchezo mmoja mkononi.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.