Kwa mujibu wa mtandao wa Pan African Footbal Klabu za Zimbabwe, FC Platinum na Bulawayo Chiefs ziko katika mvutano kuhusu usajili wa Perfect Chikwende aliyetua Simba na kupelekea kuchelewesha kutolewa kwa leseni ya kimataifa (ITC) ya mshambuliaji huyo aliyetua Simba.
Chikwende alisaini kandarasi ya miaka miwili na Simba wiki mbili zilizopita lakini bado hajapata ITC baada ya klabu yake ya zamani, Bulawayo Chiefs kukiandikia Chama cha Soka cha Zimbabwe kusitisha mchakato huo wakidai kwamba FC Platinum inapaswa kuwafidia kwa kuwa walimtoa kwa mkopo Chikwende kwenda FC Platinum.
Chikwende alipelekwa kwa mkopo FC Platinum kwa msimu wa soka wa 2019 na 2020, lakini kwa sababu ya Ligi kusimama kutokana na Covid-19, Chama cha Soka Zimbabwe kilitoa muongozo kikifafanua kwamba mikataba ambayo ilikuwa ikimalizika mnamo 2020 inapaswa kuendelea hadi 2021.
Bulawayo Chiefs wanadai wana haki ya kulipwa sehemu ya dau la uhamisho lililolipwa na Simba kwa FC Platinum.