Home Soka City mbabe mbele ya Chelsea

City mbabe mbele ya Chelsea

by Sports Leo
0 comments

Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka nchini Uingereza Manchester city wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya mabingwa watetezi wa klabu bingwa Ulaya Chelsea kwenye mchezo wa ligi kuu ya nchi hiyo hii leo.

Bao pekee la mchezo liliwekwa wavuni na kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Ubelgiji Kevin De Bruyne kwa shuti kali umbali wa takribani mita 25 nje ya penati box.

Huu unakuwa ushindi wa pili mfululizo kwenye ligi msimu huu Pep Guardiola akimtambia Thomas Tuchel wa Chelsea baada ya kocha huyo wa Kijerumani kumfunga Pep michezo mitatu mfululizo ukiwemo ule uliowapa Chelsea taji la Ulaya.

banner

Manchester city wamefikisha alama 13 zaidi ya chelsea waliopo kwenye nafasi ya pili,hali inayozifanya mbio za ubingwa wa ligi hiyo kuwa za upande mmoja tu licha ya Liverpoo aliyepo nafasi ya tatu akiwa na micheo miwili mkononi pamoja na kuzidiwa alama 14.

Mchezo mwingine wa ligi kati ya Totenham na Arsenal uliokuwa upigwe siku ya Jumapili umeahirishwa kutokana na Arsenal kuwa na idadi chache ya wachezaji kuleleka mchezo huo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited