Home Soka Congo,Morocco Matatani Caf

Congo,Morocco Matatani Caf

by Sports Leo
0 comments

Shirikisho la soka barani Afrika (Caf) limeanzisha uchunguzi maalumu juu ya vurugu zilizotokea wakati wa mchezo wa pili wa kundi F baina ya timu za Taifa za Morocco na Congo DR ambapo timu hizo zilitoka sare ya 1-1 na kuzidi kulifanya kundi hilo kutotabirika nani atapita.

Baada ya mchezo kuisha kuliibuka vurugu ambapo zilianza kwa kocha wa Morocco na Walid Regragui na beki wa DR Congo, Chancel Mbemba ambao walikunjana na kusababisha maofisa wa timu zote mbili kuingilia vurugu hizo ambazo ziliianzia uwanjani na kuendelea tena vyumbani ambapo Caf imeamua kuchunguza mashirikisho yote mawili ambapo baada ya kujiridhisha watatoa uamuzi.

Baada ya mchezo Wachezaji na maofisa walirekodiwa wakikimbilia kwenye vyumba vya kuvalia, huku aliyerekodi video hiyo akidai polisi zaidi waliitwa uwanjani hapo.

banner

Katika mchezo huo Morocco walipata bao kupitia Achraf Hakimi dakika ya 6 ya mchezo akiunganisha mpira wa kona huku Congo DR wakisawazisha bao hilo dakika ya 70 kupitia kwa Silas Katompa Mvumpa na kupelekea kugawana alama kwa timu hizo zilizojaa mastaa.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited