Home Soka Costa Anukia Ureno

Costa Anukia Ureno

by Sports Leo
0 comments

Kuna uwezekano mkubwa wa staa wa zamani wa Atletico Madrid na Chelsea Diego Costa kujiunga na timu ya Benfica Fc inayoshiriki ligi kuu nchini Ureno baada ya klabu hiyo kukubaliana na wakala George Mendez anayemsimamia mchezaji huyo.

Awali staa huyo aliyechagua kuichezea timu ya taifa ya Hispania badala ya Brazil alivunja mkataba na timu ya Atletico Madrid kwa makubaliano ya pande mbili huku akiwa na mawazo ya kurejea Brazil lakini uhusiano mzuri wa Mendez na Benfica umesababisha staa huyo kubadili mawazo.

Costa atalipwa kiasi cha paundi milioni 2.6 kwa mwaka katika mkataba wa miaka miwili atakaosaini katika klabu hiyo maarufu barani ulaya.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited