Beki wa klabu ya Yanga Andrew Vicent “Dante” ameiwekea ngumu klabu hiyo kumlipa fedha zake kwa awamu kama inavyofanya kwa mastaa wengine huku akihitaji kulipwa zote kwa mkupuo mmoja.
Staa huyo anaidai timu hiyo kiasi cha shilingi milioni 40 ikiwa ni fedha za usajili pamoja na mishahara ameombwa na klabu hiyo kukubali kulipwa kwa awamu tatu ambapo awamu mbili atalipwa milioni 15 na awamu ya mwisho atalipwa milioni 10.
Kwa mujibu wa Afisa Habari wa klabu hiyo Michael Bumbuli staa huyo amegoma akihitaji kulipwa fedha zote kwa mkupua mmoja tofauti na ilivyokua kwa mastaa wengine akiwemo Juma Abdul ambaye amejiunga na timu hiyo baada ya kukubali kulipwa kidogo kidogo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.