Beki wa klabu ya Yanga sc Andrew Vicent “Dante” amegoma kujiunga na timu hiyo akishinikiza kulipwa fedha za usajili anazoidai timu hiyo.
Beki huyo aliyejiunga na timu hiyo akitokea Mtibwa sugar amejiondoa katika timu hiyo akishinikiza alipwe madai hayo ya fedha za usajili za miaka miwili iliyopita ambapo inasemekana fedha hizo zinakaribia shilingi milioni 45.
Kocha Mwinyi Zahera alisisitiza madai ya beki huyo kushughulikiwa baada ya kujitoa kwa msimu uliopita kuipambania timu hiyo ilipokua na hali ngumu kiuchumi.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
“Milango iko wazi kurejea kama anaweza kukubali kulipwa kidogo kidogo”alisema makamu mwenyekiti wa klabu hiyo David Mwakalebela.