Kiungo Salum Abubakary na Mshambuliaji Prince Dube wa Azam fc wametwaa tuzo za wachezaji bora wa mwezi Septemba na Oktoba wa klabu hiyo yenye maskani yake Chamazi jijini Dar es salaam.
Tuzo hizo walikabidhiwa kabla ya kuanza kwa mchezo baina ya timu hiyo na Dodoma jiji Fc ambao Azam fc waliibuka na ushindi wa mabao 3-0.
Sure boy alitwaa tuzo hiyo akiwashinda wachezaji wenzake, beki Bruce Kangwa, kiungo mkabaji Ally Niyonzima, washambuliaji Obrey Chirwa na Prince Dube,Huku Dube akiwashinda David Kissu,Abdallah Kheri,Bruce Kangwa na Salum Abubakary.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Tuzo hiyo walikabidhiwa na Sheikh Twalib, kabla ya kuanza kwa mchezo kati ya Azam FC na Dodoma Jiji uliochezwa jana Novemba 5.