Home Soka Fati,Torres fit kuwavaa Madrid

Fati,Torres fit kuwavaa Madrid

by Sports Leo
0 comments

Kocha wa FC Barcelona Xavi Hernandes amepata ahueni baada ya jopo la madaktari wa klabu hiyo kuwaruhusu wachezaji Ansu Fati na Ferren Torres kucheza mchezo wa leo wa nusu fainali ya super cup dhidi ya Real Madrid.

Ansu Fati aliumia mwishoni mwa mwaka jana kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Valencia walioshinda 2-1 na amekuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi miwili huku hajacheza mechi hata moja chini ya kocha mpya wa timu hiyo Xavi.

Kinda huyo bado anabeba matumaini ya mashabiki wa Barcelona katika kipindi hiki kigumu wanachopitia tangu kuondoka kwa Messi.

banner

Naye mshambuliaji mpya aliyesajiliwa kutoka Man city Ferran Torres yupo tayari kucheza mchezo wake wa kwanza ndani ya uzi wa miamba hiyo kutoka Nou Camp mara baada ya kupona majeraha yake pamoja na kusajiliwa rasmi ndani ya shirikisho la soka nchini Hispania.

Mchezo huo wa E l Classico utafanyika hii leo majira ya saa nne usiku huku wadau wa soka wakisubiri kuona ni nini Xavi atafanya kutokana na timu hiyo kuwa wateja wa wapinzani wao wakuu katika misimu hii mitatu ya hivi karibuni wakifungwa michezo mitano iliyopita.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited