Nyota wa nne wa timu ya Yanga wamerejea kikosini tayari kuongeza nguvu kuelekea mchezo wa Jumapili wa Ligi Kuu dhidi ya Azam FC.
Nahodha Lamine Moro, Feisal Salum na Dickson Job ambao walikuwa marejeruhi wamerejea kikosini na jana wamefanya mazoezi pamoja na wenzao.
Mlinda mlango Metacha Mnata aliyekuwa na matatizo ya kufiwa na mtoto wake nae amerejea kikosini.
Msemaji wa klabu hiyo, Hassan Bumbuli amesema wanafahamu mchezo utakuwa mgumu kutokana na ubora wa Azam huku wakijinasibu kuondoka na alama zote tatu.
“Tunahitaji kushinda mechi zetu zote za Ligi zilizobaki, tunajua mchezo utakuwa mgumu lakini tupo tayari kwa mchezo na tuna uhakika wa kubaki na alama zote tatu,” amesema Bumbuli.