Afisa habari wa klabu ya Yanga sc Hassan Bumbuli amesema kuwa klabu hiyo itawakosa viungo wake mahiri Feisal Salum na Mukoko Tonombe kutokana na kadi tatu za njano walizozipata katika michezo ya ligikuu nchini.
Pia Bumbuli amesema kuwa pamoja na viungo hao pia mshambuliaji Michael Sarpong nae atakosekana katika mchezo huo kutokana na kadi tatu kama wenzake.