Pep Guardiola amedai kwamba Manchester City huenda ikamfuta kazi iwapo watashindwa kuilaza Real Madrid katika kombe la mabingwa Ulaya katika mchezo utakaochezwa february 26 mwaka huu.
Hata hivyo kufutwa kazi kwa Guradiola sio kitu rahisi kutokana na rekodi yake bora aliyoiweka baada ya kushinda mataji matano muhimu licha ya kushindwa kuiepeleka mbele ya robo fainali ya kombe la klabu bingwa katika misimu mitatu.
Guardiola alijiunga na Man city akitokea Bayern Munchen na licha ya kuwa na mafanikio katika timu mbalimbali alizofundisha hali imeonekana kuwa ngumu klabuni hapo baada ya kuwa na msimu mgumu huku akielekea kupoteza ubingwa wa ligi kwa Liverpool.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.