Paris st.German(PSG) wamekamilisha usajili wa kiungo msenegali Idrissa Gana Gueye kutoka klabu ya Everton kwa dau la paundi milioni 29 kwa mkataba wa miaka minne huku kukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi.
Kiungo huyo alisajiliwa na Everton akitokea Aston Villa kwa dau la paundi milioni 7.1 miaka mitatu iliyopita chini ya waliokua makocha wa timu hiyo Roenad Koeman na Steve Walsh na sasa amekamilisha uhamisho huo ambao ulishindikana msimu uliopita baada ya wababe hao wa Ufaransa kushindwa kufikia dau lililohitajika na Everton.
Taarifa zinadai tayari mchezaji huyo yuko mjini Paris kwa ajili ya utambulisho rasmi na taratibu zingine.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Gueye alikua na msimu mzuri akiwa na Everton huku akionyesha kiwango bora katika michuano ya Afcon akiwa na timu ya taifa ya Senegal ambao walifungwa mechi ya fainali na Algeria.