Staa wa klabu ya Simba sc Deo Kanda amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Yanga sc utakaofanyika jioni ya leo katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Kanda amesema kuwa licha ya Yanga kuwa na mabeki imara wakiongozwa na Kelvin Yondan hilo haliwatishi na kushindwa kuibuka na ushindi katika mchezo huo wa ligi kuu.
“Tunakwenda kucheza na Yanga ni wazuri wameimarika hasa eneo la ulinzi ila hilo haltufanyi tushindwe kufanya vizuri.Tunajua ngome hiyo inamtegemea Yondani na wenzake lakini kama washambuliaji tupo vizuri mno na hawataamini tutakachowafanyia taifa kwenye dabi.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kanda amesajiliwa na Simba kwa mkopo akitokea Tp Mazembe ya kongo na siku za karibuni amekua na kiwano bora akifunga mabao mawili katika mechi mbili mfululizo.