Home Soka Kane Kuipasua Man Utd

Kane Kuipasua Man Utd

by Sports Leo
0 comments

Mshambuliaji wa klabu ya Tottenham Harry Kane ataigharimu Manchester United kiasi cha Paundi milioni 200 ili kukamilisha usajili wa kujiunga na klabu hiyo.

Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali ya michezo barani ulaya Mtendaji mkuu wa klabu ya Tottenham Daniel Levy yuko tayari kumpiga bei staa huyo kwa bei hiyo ili kuweka sawa vitabu vya fedha klabuni hapo ambavyo vimeyumba kutokana na masuala mbalimbali ikiwemo kusimamishwa kwa ligi kutokana na ugonjwa wa Covid-19.

Licha ya uamuzi wa mkurugenzi huyo bado kocha wa klabu hiyo Jose Mourinho amekiri bado anamhitaji staa huyo ambaye pia ni tegemeo katika timu ya taifa ya Uingereza.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited