Kamati ya waamuzi wa mpira wa miguu nchini imemteua mwamuzi Ramadhani Kayoko kutoka Dar es salaam kuchezesha mechi ya ngao ya hisani kati ya watani wa jadi Simba na Yanga utakaofanyika jumamosi hii katika uwanja wa Benjamin Mkapa.
Kayoko ni mmoja kati ya waamuzi bora kwasasa nchini akifanya vizuri misi mu miwili iliyopita tangu alipochaguliwa kucheza michezo ya ligi kuu soka Tanzania Bara.
Hivi karibuni Kayoko aliteuliwa na shirikisho la soka Afrika (CAF) kuchezesha mechi za kombe la shirikisho ikiwa ni ishara ya uwezo mzuri anaouonyesha dimbani.
Hata hivyo hii haitakuwa mara ya kwanza kwa mwamuzi huyo kuchezesha mechi hiyo kubwa kabisa Tanzania na Afrika kwani alifanya hivyo msimu wa 2019/2020 ambao alichaguliwa kuwa mwamuzi bora wa msimu na alipongezwa kwa kumudu vyema presha ya mchezo huo.
Katika kuthibitisha kuaminiwa na vilabu vyote viwili Ramadhani Kayoko alichezesha mechi kati ya Yanga na Zanaco katika kilele chwa wiki ya Mwananchi August 29 mwaka huu kabla ya Simba nao kumpa jukumu la kuchezesha mechi yao dhidi ya TP Mazembe kwenye Simba day Septemba 19.
Kaayoko atasaidiwa na Frank Komba (line one),Soud Rila (line two) na Heri Sasii ambaye atakuwa mwamuzi wa akiba
Â