Timu ya Taifa ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) imekubali kipigo cha bao moja kutoka kwa Harambee Stars katika mchezo wa michuano ya chalenji uliofanyika katika uwanja wa KCCA nchini Uganda.
Kenya walifanikiwa kupata bao pekee la mchezo huo dakika ya nne ya mchezo likifungwa na Hassan Abdalah baada ya mabeki wa Stars kuzembea.
Bao hilo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo licha ya Stars kujitahidi kutafuta goli la kusawazisha lakini uimara wa mabeki wa kenya ulikua mwiba kwa washambuliaji wa Stars wakiongozwa na Paul Nonga.