84
Kocha wa Taifa Stars Kim Poulsen amelibakisha benchi lote la ufundi lilokuwa likitumiwa na Ettienne Ndayilagije wakiwemo makocha wasaidizi Selamani Matola na Juma Mgunda.
“Benchi la ufundi litabaki lilelile kama lilivyokuwa, nilikuwa na mazungumzo mazuri na Mgunda pamoja na Matola lakini pia nimeshakutana na Matola na tumeongea”.Alisema Kim
“Pamoja na kocha wa makipa na kocha wa viungo watabaki vilevile sikuona sababu ya mimi kuja hapa na kubadilisha kila kitu, ingawa akija kocha mpya anaangalia ni kivipi unafanya kazi yako, kikubwa kila mtu atimize majukumu yake vizuri kuanzia kwa wachezaji hadi benchi la ufundi,”
Kwa sasa Matola ni kocha msaidizi wa klabu ya Simba, huku Mgunda akiwa kocha mkuu wa klabu ya Coastal Union.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.