Kocha wa timu ya Yanga sc Mkongomani Mwinyi Zahera ameweka bayani kuwa usajili wa mshambuliaji mpya wa klabu hiyo aliyetua jana usiku atachukua nafsi ya kipa Klaus Nkizi Kindoki atakayerudishwa Fc Lupopo.
Kocha huyo amesema kuwa Kindoki atarudishwa Kongo ili kutoa nafasi ya usajili wa David Molinga(Falcao) ili kukidhi hitaji la wachezaji kumi wa kigeni kama kanuni zinavyotaka.
“Mchezaji huyu ametokea Kongo kwenye timu waliyotokea Makambo na Kindoki na tulishafanya mazungumzo na Kindoki kuwa atarudi kule Lupopo akaive sawasawa hivyo hakuna utata kila kitu kipo sawa”Alisema Zahera.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kuondoka kwa kipa huyo klabuni kunamaanisha timu hiyo itabaki na makipa watatu,Mkenya Farouk Shikalo na wazawa Metacha Mnata na Ramadhani Kabwili.