Home Soka Kipa Azam Fc Ahitajika Sudan

Kipa Azam Fc Ahitajika Sudan

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Al Hilal ya Sudan inampango wa kumrejesha Kipa wake anayekipiga Kwa mkopo wa nusu msimu ndani ya klabu ya Azam Mohammed Mustafa mwishoni mwa msimu huu kutokana na kuwa na mahitaji naye kwa ajili ya msimu ujao.

Kipa huyo alisajiliwa na Azam Fc kwa mkopo kuja kuziba nafasi zilizoachwa wazi na makipa Ali Ahmada na Abdulai Iddrisu ambao wote wawili ni majeruhi wa muda mrefu ambapo hadi sasa kipa huyo amekua akisaidiana na Zubeiry Foba kulinda lango la Azam Fc

Kujiandaa na hilo tayari klabu ya Azam  Fc imekamilisha mazungumzo na kipa wa klabu ya Tabora United raia wa Nigeria John Noble ambaye anatarajiwa kujiunga na timu hiyo msimu ujao baada ya kumaliza kandarasi yake na Tabora United.

banner

Azam Fc imeendelea kujenga kikosi kikali cha ushindani ikifanikiwa kufanya sajili chache na muhimu kikosini humo akiwemo Feisal Salum sambamba na Yannick Bangala huku ikifanikiwa kuwalinda mastaa kadhaa kwa kuwaongezea mikataba.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited