Home Soka Kisasi ni Haki-Yanga sc

Kisasi ni Haki-Yanga sc

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Yanga sc imepanga kulipiza kisasi cha kutolewa katika michuano ya kimataifa msimu huu katika hatua ya robo fainali baada ya kupangwa na Rivers United ya Nigeria ambayo iliwatoa katika hatua ya awali ya michuano hiyo miaka miwili iliyopita.

Katika droo hiyo ambayo ilifanyika usiku ya kuamkia alhamis ya leo Yanga sc imepangwa na Rivers United katika hatua ya robo fainali ambapo itaanzia ugenini nchini Nigeria kisha itamalizia nyumbani nchini Tanzania na ikifuzu basi itakutana na mshindi kati ya Pyramid Fc ya nchini Misri na Malumo Gallants ya Afrika ya Kusini.

Wadau wengi wa soka wameipa nafasi Yanga sc kutokana na kiwango chao cha siku za hivi karibuni ugenini na nyumbani huku pia wakiwa na faida ya kuanzia ugenini.

banner

“Kwanza tulikua tunaisubiri hii droo kwa hamu na nimefurahi kukutana nao kwa maana mwaka juzi sikupata nafasi ya kucheza nao na tulitolewa mapema na watu waliongea sana”.

Ali Kamwe ambaye ni Afisa habari wa klabu hiyo yeye alisisitiza kuwa mechi hiyo ni ya kulipa kisasi huku akitambulisha kauli mbiu ya “Kisasi ni Haki”.

Mchezo huo ya robo fainali inatarajiwa kufanyika kati ya April 21-23 nchini Nigeria huku marudiano ikiwa ni kati ya tarehe 28-30 April nchini Tanzania.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited