Klabu ya Simba SC imekamilisha usajili wa Kiungo Babacar Sarr raia wa Senegal kama Mchezaji huru baada ya kuachana na Monastir ya Tunisia ambapo amesaini mkataba wa miaka miwili na nusu kukipiga katika klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Msimbazi jijini Dar es salaam.
Kiungo huyo kabla ya kuja Simba Sc alikua anaichezea klabu ya Us Monastir ya nchini Tunisia ambapo walishiriki Arab Club Champions Cup na kucheza na Al Nassr mchezo ambao walifungwa mabao 4-1 huku staa Cristiano Ronaldo naye akicheza mchezo huo.
Simba sc imepata mtelezo kumsajili staa huyo kutokana na kuwa hana timu tangu mwezi Novemba baada ya kuachana na Us Monastry ambayo aliichezea kwa miezi sita pekee akicheza michezo saba na kufunga goli moja.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Staa huyo anakuja kujibu ombi la kocha Abdelhack Benchika ambaye alikua anahitaji kiungo mkabaji baada kutoridhishwa na ufanisi wa viungo aliowakutana klabuni hapo.