Kocha wa timu ya Pamba fc inayoshoriki ligi daraja la kwanza Muhibu Kahn amechana na timu hiyo baada ya kuandika barua uongozi wa kuomba kuachana na timu hiyo,Taarifa Rasmi kutoka katika klabu hiyo inasomeka ifuatavyo.
Uongozi wa Klabu Ya Pamba SC Tumefika Makubaliano ya Kuvunja Mkataba na aliyekua Kocha Wetu Muhibu Kanu kwa makubaliano ya Pande zote Mbili Baada ya Ombi lake la Kuvunja Mkataba kukubaliwa na Kamati tendaji Ya Klabu.
Kocha Muhibu Aliomba Kuondoka kwenye Klabu kutokana na Sababu zilizo Nje ya Uwezo wake na Uongozi Leo hii Umefika makubaliano ya Kuachana na Kocha huyo na mchakato wa kumpata Kocha Mpya Ukiwa tayari Umeanza.
Hata Hivyo Uongozi wa Klabu ya Pamba SC umeamua Kuvunja Benchi lake la Ufundi na Kuacha majukumu ya Kuongoza katika Mazoezi Chini ya Kocha wa Makipa Hassan Shehata.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Pamba SC inamtakia Kila lakheri Kocha Muhibu Kanu na tunamshukuru kwa mchango wake Wote ndani ya Klabu yetu.