Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael atawasili kesho Jumatano saa 7:20 mchana tayari kuungana na kikosi kwa ajili ya mwendelezo wa mechi za Ligi na Kombe la FA akitokea nchini Ubeligiji alikokua mapumzikoni baada ya ligi kusimamishwa kufuatia kusambaa kwa maambukizi ya Virusi vya Corona nchini.
Luc anatarajiwa kuwasili kesho saa saba mchana baada ya kuchelewa kupata ndege kufuatia nchi nyingi duniani kufunga mipaka na anga la ndege.
Taarifa za kocha huyo kuwasili nchini zimethibitishwa na klabu ya Yanga kupitia mtandao wa Yanga App ambako mpaka sasa zaidi wananchama 26000 wamejiunga kupata habari za klabu hiyo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.