Baada ya kutupwa nje ya mashindano ya Cecafa wanawake 2019 Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Queen’s Mohammed Ally salah amesema kuwa kitendo cha kikosi chao kuruhusu magoli 17 katika msimu huu wa Cecafa ni hatua kubwa sana kwao kulinganisha Cecafa iliyo pita ambayo waliruhusu magoli 31
Ameongeza kuwa wanarudi nyumbani kujipanga kuitengeza timu kwa kushirikiana na shirikisho la soka visiwani Zanzibar ZFA katika kuianzisha ligi ya wanawake visiwani humor ili kuijenga Zanzibar Queen’s imara na yenye kuleta ushinda katika mashindano ya Cecafa yajayo
Katika michezo mitatu ya Zanzibar hatua ya nakundi akiwa kundi A mechi ya kwanza alifungwa goli 5 na Burundi huku mechi ya pili wakaifunga Sudani goli 5 na mechi ya tatu wamefungwa na Kilimanjaro Queen’s (Tanzania) goli 7.