Nguli wa mziki wa Bendi barani Afrika Koffi Olomide ametua nchini ambapo atasherehesha tukio la siku ya wananchi liliandaliwa na klabu ya Yanga sc ikiwa ni siku maalumu ya kufanya utambulisho wa wachezaji wapya kwa ajili ya msimu wa ligi kuu nchini 2021/2022.
Koffi akiwa sambamba na wasaidizi wake ametua leo uwanjani na kupokelewa na afisa habari mpya wa klabu ya Yanga sc Haji Manara aliyekua na kundi la mashabiki kadhaa waliojitokeza kumpokea mwanamuziki huyo mkubwa mwenye vibao vikali.
Mpaka sasa tiketi za tamasha hilo zimenunuliwa kwa wingi na mashabiki wa klabu hiyo huku tayari tiketi za watu mashuhuri zikiwa zimeisha zikibaki za watu mashuhuri daraja la tatu na mzunguko ambazo zinauzwa elfu 20 na elfu 5.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.