Home Soka Leicester yaipunguza kasi Liverpool

Leicester yaipunguza kasi Liverpool

by Dennis Msotwa
0 comments

Leicester city wameizuia Liverpool kuendelea kuwabana kileleni vinara Manchester city baada ya usiku wa kuamkia leo kuwapa kipigo cha 1-0 kwenye mchezo wa ligi kuu soka nchini Uingereza.

Bao pekee la mchezo liliwekwa kimiani na winga hatari Ademola Lookman kunako dakika ya 59 baada ya kumalizia kazi nzuri ya kiung Dewsburry Hall.

Liverpool wangeweza kupata bao la uongozi kipindi cha kwanza baada ya kupata penati,hata hivyo mshambuliaji Mohamed Salah alikosa mkwaju huyo ukiokolewa na golikipa Kasper Schmeichel na licha ya mpira kurudi kwa Salah lakini bado pia alishindwa kuweka kimiani.

banner

Kwa matokeo hayo sasa Manchester city wanaendelea kjikita kileleni kwa tofauti ya pointi sita nyuma ya Liverpool na Chelsea waliofungana alama,huku city wao wakishuka dimbani Jumatano hii kucheza dhidi ya Brentford.

Matokeo mengine ya ligi hiyo kwa mechi za jana: Southampton 1-1 Tottenham, Watford 1-4 West Ham,Crystal Palace 3-0 Norwich.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited