Mshambuliaji wa kitanzania Elias Maguli amejiunga na FC Platinum ya Zimbabwe kwa kandarasi ya miaka 2 kuvunja mkataba na klabu yake ya awali ya Nakambala Leopard ya Zambia.
Staa huyo aliyewahi kuzichezea timu za Stand United,Ruvu Shooting,Simba,Prisons na Kmc za hapa nchini ametambulishwa rasmi ndani ya timu hiyo baada ya kukamilisha uhamisho huo.
Pia Maguli amewahi kuzichezea timu ya Dhofar iliyopo katika ligi kuu nchini Oman kabla ya kutimka na kurudi nchini.